
Watu watano wanaosadikiwa kuwa ni majambazi wakiwa na silaha wamevamia nyumba tatu katika Kijiji cha Nyamidaho wilayani Kasulu mkoani Kigoma na kumuua kwa kumpiga risasi Mfanyabiashara Daglas Kingunyi na kupora fedha na bidhaa mbalimbali kwenye maduka mawili katika Kijiji hicho ambapo Kamanda wa Polisi mkoani humo Kamishana Msaidizi wa Polisi, James Manyama amebainisha kuwa Mfanyabiashara huyo alifariki wakati akipelekwa hospitali na wanaendelea na oparesheni ya kuwasaka wahalifu hao.
