Back to top

Mfanyabiashara wa Uganda mbaroni kwa kutaka kitambulisho cha Taifa

13 January 2020
Share

Idara ya uhamiaji katika mkoani Kagera imemkamata mfanyabiashara raia wa  Uganda, Frank Mpuuga akiwa katika harakati za kukamilisha taratibu za kuomba kitambulisho cha taifa.

Aidha idara hiyo pia  inamshikilia Swalehe Athumani Mtanzania anayedaiwa kumuingiza kinyemela nchini mfanyabiashara huyo  na kumpa mbinu za kuomba kitambulisho hicho.

Baada ya kupekuliwa mfanyabiashara huyo alikutwa na hati ya kusafiria ya Uganda.
Mkuu wa mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco Elisha Gaguti ametoa onyo kwa wale wote wenye nia ya kujipatia vitambumbulisho vya taifa wakati sio watanzania na ameagiza watu wawili waliokamatwa wachukuliwe hatua kali ili liwe fundisho kwa wengine.