Back to top

Mfuko wa Maendeleo Abu Dhabi kufadhili miradi Tanzania.

29 September 2022
Share

Mfuko wa Maendeleo wa Abu Dhabi umeahidi kutoa mkopo nafuu kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo nchini Tanzania ukiwemo mradi wa umeme wa Benaco-Kyaka, mkoani Kagera na ujenzi wa makazi ya watumishi ya gharama nafuu Visiwani Zanzibar, inayokadiriwa kugharimu dola za Marekani milioni 420. 

Ahadi hiyo imetolewa Mjini Abu Dhabi na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Maendeleo wa Abu Dhabi (, Mhe. Mohammed Saif Al Suwaidi, wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba, Makao Makuu ya Mfuko huo, mjini Abu Dhabi, Umoja wa Falme za Kiarabu.