
Moja ya Mawakili wa Aliyekuwa Mgombea wa Azimio la Umoja katika uchaguzi Mkuu nchini Kenya Raila Odinga, Bw.Philip Murgor amedai kwamba kulikuwa na kundi la watu 50 katika mtaa wa Karen ambao walivuruga mitambo ya TEHAMA ya Tume Huru ya Uchaguzi ya Mipaka (IEBC), na kubadilisha matokeo ya kura za Urais kabla ya kupachikwa tena kwenye mfumo wa IEBC.
.
Wakili huyo amebainisha kuwa wana ushahidi wa kutosha kuwa mfumo wa IEBC ulivurugwa na watu wasiojulikana ambapo amewataja watu watatu wa Venezuela ambao walitiwa mbaroni kabla ya kuandaliwa kwa uchaguzi mkuu wakiwa na vifaa vya Tume ya IEBC, na kwamba waliweza kuingia katika mifumo ya Tume hiyo.
