Back to top

Mfumuko wa bei wa taifa kwa mwezi Julai 2018 wapungua.

09 August 2018
Share

Ofisi ya Taifa ya Takwimu NBS imetangaza kupungua kwa kasi ya  bei kwa bidhaa na huduma mbalimbali kwa mwezi julai mwaka huu hadi kufikia asilimia 3.3 kutoka asilimia 3.4 ya mwezi Mei mwaka 2018 kiwango ambacho hakijawahi kutokea nchini kwa miaka 17 iliyopita.

Akitangaza mfumuko wa bei wa taifa jijini Dodoma mkurugenzi wa sensa ya watu na takwimu za jamii bw Ephraim Kwesigabo amesema kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia mwezi Julai mwaka huu imepungua ikilinganishwa na kasi iliyokuwa kwa mwaka ulioishia mwezi  Juni 2018.

ITV imetembea katika baadhi ya masoko ya jiji la Dodoma na kuzungumza na wafanyabiashara ambapo wamekiri kushuka kwa bei za bidhaa mbalimbali za masoko ambapo wamesema kuwa licha ya kushuka kwa bei hizo kwao imekuwa ikiwaathiri kiuchumi.