Back to top

MFUMUKO WA BEI WA TAIFA WAPUNGUA HADI 3.0%

09 January 2024
Share

Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa mwaka ulioishia mwezi Disemba 2023, umepungua hadi 3.0%, kutoka 3.2% kwa mwaka ulioishia mwezi Novemba 2023.
.
Taarifa hiyo imetolewa na Ofisi ya Takwimu ya Taifa ambapo imebainisha kuwa kupungua kwa mfumuko huo kumesababishwa na kupungua kwa mfumuko wa bei wa baadhi ya bidhaa za vyakula na bidhaa zisizo za vyakula kwa kipindi cha mwaka ulioishia mwezi Disemba 2023.
.
Baadhi ya bidhaa za vyakula zilizoonesha kupungua ni pamoja na mchele ambao umepungua kutoka 2.6% hadi 0.5%, samaki (kutoka 5.1% hadi 2.5%), dagaa (kutoka 12.7% hadi 5.8%), matunda (kutoka 5.7% hadi 2.4%), mbogamboga (kutoka 12.9% hadi 9.1%) na njegere (kutoka 5.9% hadi 2.8%).