
Bunge la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo limepiga kura ya kumuondoa Waziri wa Uchumi wa nchi hiyo Jean-Marie Kalumba kutoka kwenye wadhifa wake, likimlaumu kupanda kwa bei ya bidhaa za kimsingi na usimamizi mbovu wa sekta ya uvuvi.
.
Waziri huyo aliyeteuliwa kushika wadhifa huo na Rais wa nchi hiyo Felix Tshisekedi, mwaka jana amepewa masaa 48 za kuwasilisha barua yake ya kujiuzulu.
