Jeshi la polisi mkoa wa Mara linawashikilia watu watano kwa tuhuma za ujambazi akiwamo mganga wa kienyeji ambaye anadaiwa kuwalinda watuhumiwa hao kwa kuwapa dawa za kienyeji ili wasikamatwe wala kujulikana pale wanapofanya uhalifu.
Akizungumza na waandishi wa habari Kamanada wa jeshi la polisi mkoa wa Mara ASP Daniel Shillah amesema watuhumiwa hao wamekamatwa wilaya ya Butiama wakiwa na mganga wao.