Back to top

MGANGA MFAWIDHI KIVULE AVULIWA MADARAKA

09 July 2023
Share

Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya Kivule amevuliwa madaraka kufuatia kusambaa kwa video iliyomuonyesha mtumishi wa Hospitali hiyo akiosha na kuanika juani, vifaa tiba nje ya jengo la hospitali, kitendo ambacho ni kinyume na taratibu na miongozo ya afya.
.
Hatua hiyo imechukuliwa na Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam Jomari Satura, ambapo ameomba radhi kwa Mamlaka na umma wote wa Watanzania kwa kitendo hicho kilicholeta usumbufu na taharuki.
.
Aidha, Satura amemuagiza Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam, kuhakikisha anasimamia kwa ukaribu utoaji wa huduma katika vituo vyote vya kutolea huduma za afya vya Serikali na binafsi. #mwananchi