
Mgodi wa Barrick North Mara uliopo mkoani Mara umepigwa faini ya shilingi Bilioni moja na Baraza la Taifa la Uhifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kwa kosa la uchafuzi wa mazingira baada ya bomba linalopitisha maji taka kutoka kwenye mgodi huo kupasuka na kutiririsha maji katika Mto Tigite unaomwaga maji yake mto Mara.
