Back to top

Mgogoro uliodumu kwa miaka mitatu watatuliwa na waziri Mhe.Biteko

08 December 2019
Share

Serikali kupitia wizara ya madini imetatua mgogoro wa muda mrefu wa wachimbaji wadogo katika mgodi mkubwa wa zamani unaojulikana kwa jina la Resolute ulioko katika wilaya ya Nzega mkoani Tabora kwa kugawa leseni 11 kwa wachimbaji wadogo ili waendelee kutumia eneo hilo la mgodi ambao awali ulifungwa kuchimba madini ya dhahabu.


Akizungumza baada ya kugawa wa leseni hizo kwa vikundi 11 vya wachimbaji wadogo ambao wamekuwa wakililia kupewa maeneo katika mgodi huo wa Resolute ambao umefungwa kwa zaidi ya miaka mitatu waziri wa madini Dotto Biteko amewataka wachimbaji hao kuachana na migogoro isiyo na lazima na kujenga tabia ya kulipa kodi ya serikali kwa wakati.


Naye mkuu wa wilaya ya Nzega Godfrey Ngipula amesema sheria na taratibu za uchimbaji ni lazima zifuatwe huku mkurugenzi wa leseni nchini Yahya Samamba akitilia mkazo kwa wachimbaji kutumia vyema fursa ya leseni walizopewa.