Back to top

MGOGORO WA ARDHI SAGARA WATATULIWA.

15 October 2023
Share

Waziri wa Ardhi Mhe Jerry Silaa, amesema eneo la Sagara wilaya ya Singida mkoani Singida halina mgogoro wa ardhi baada ya mgogoro uliokuwepo eneo hilo kutatuliwa.

Waziri Silaa ametoa kauli hiyo mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan, alipopewa nafasi ya kusalimia wananchi wakati wa mwanzo wa ziara ya Rais ya siku tatu mkoani Singida.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan, ameanza ziara yake ya siku tatu ambapo mbali na mambo mengine katika ziara yake atapokea taarifa ya mradi wa ujenzi wa shule zilizopokea fedha kupitia miradi ya BOOST, SEQUIP na Serikali Kuu, ataweka jiwe la msingi ujenzi wa barabara ya Mkiwa-Itigi-Noranga km 56.9 kwa kiwango cha lami pamoja na kuweka jiwe la msingi katika kituo cha polisi Ikungi.