Back to top

Mgombea Urais wa upinzani nchini Uganda Bobi Wine Akamatwa na Polisi.

18 November 2020
Share

Kiongozi wa chama cha National Unity Platform (NUP) Robert Kyagulanyi Maafufu Bobi Wine amekamatwa na jeshi la polisi nchini Uganda akiwa katika harakati za kampeni.

Bobi wine amekamatwa na maafisa wa polisi katika wilaya ya Luuka mashariki mwa Uganda,alikokuwa anatarajiwa kuendesha kampeni.

Maafisa wa usalama wanamshutumu kwa kuendesha mikutano ya hadhara bila kuzingatia masharti ya kudhibiti maambukizi ya homa ya Corona.

Bobi Wine akiwa ndani ya gari la Polisi baada ya kukamatwa nchini Uganda.

Msemaji wa idhara ya polisi Fred Enanga ametangaza kwamba mgombea yeyote atakaye endesha mikutano ya kampeni za hadhara atakamatwa, hata hivyo haijajulikana mpaka sasa mwanamuziki huyo amepelekwa wapi na polisi.

Zaidi bonyeza Video hapa.