Back to top

Mgomo wa vijana wa JKT wamsikitisha mkuu wa Majeshi.

18 April 2021
Share

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jen.Venance Mabeyo amesema amesikitishwa na vijana 854 wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) ambao wamekiuka taratibu kwa kuanzisha mgomo na kufanya maandamano ya kwenda Ikulu kwa madai ya kutaka kumuona Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu ili wadai kuandikishwa Jeshini kama walivyoahidiwa na aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Dkt. John Pombe Magufuli.

Vijana hao ni kati ya vijana 2,400 walioahidiwa kuandikishwa Jeshini na walifanya uamuzi huo baada ya Jeshi kuamua kuwapunguza katika kazi ya ujenzi wa Ikulu Chamwino baada ya kazi kupungua ili waende kufanya katika kazi maeneo mengine, lakini wao wakapinga kwa madai wangekosa kuandikishwa Jeshini.

Jen. Mabeyo amesema Jeshi halikuwa na lengo hilo na limelazimika kusitisha mikataba yao kwa kuwa kosa walilolifanya ni sawa na uasi na kwamba halivumiliki. 

Ameongeza kuwa pamoja na kufanya uchunguzi zaidi wa kwa nini walifanya hivyo Jeshi limeamua kutafakari upya mpango wa kuchukua vijana wa kujitolea kwa ajili ya kujiunga na JKT.