Mgonjwa wa kwanza wa Corona afariki Tanzania

Waziri wa Afya Mhe.Ummy Mwalimu amethibitisha kifo cha kwanza cha mgonjwa wa COVID-19 kilichotokea alfajiri ya tarehe 31 Machi 2020 katika kituo cha matibabu ya wagonjwa wa COVID -19 Mloganzila jijini Dar es Salaam.

Taarifa hiyo ya Waziri wa afya inasema, Marehemu ni Mtanzania, mwanaume, mwenye umri wa miaka 49 ambaye pia alikuwa akisumbuliwa na maradhi mengine.

Hadi kufikia alfajiri ya tarehe 31 Machi 2020 jumla wa watu waliopata maambukizi ya COVID-19 nchini Tanzania ni 19 ,aliyepona ni mmoja(1)  na kifo kimoja(1).