Back to top

Mhandisi aswekwa ndani kwa kutafuna bilion tatu za mradi wa maji.

13 December 2019
Share

Waziri wa Maji, Prof. Makame Mbarawa ameamuru Jeshi la Polisi kumkamata na kumuweka mahabusu Mhandisi Alistides Kanyomo wa kampuni ya Mbesso Construction kutoka Jijini Dar es Salaam kwa tuhuma za ubadhirifu wa zaidi ya shilingi bilioni tatu za Ujenzi wa mradi wa Maji Katika Bonde la Mwakaleli wilayani Rungwe na kusababisha wananchi katika vijiji 18 vya Halmashauri za  Busokelo na Rungwe kukosa Maji kwa kipindi cha miaka 11.         

Prof.Makame amechukua uamuzi huo baada ya kutembelea kibanda cha ofisi ya muda ya kampuni hiyo ambacho kimejengwa kwa mabati na kudaiwa kuwa Ujenzi wake umegharimu shilingi milioni 100.