Back to top

Mhe. Rais Samia afanya uteuzi wa viongozi 2.

08 June 2021
Share

Rais Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa viongozi wawili ambao ni Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) na Mjumbe wa Baraza la Ushindani.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Gerson Msigwa, Rais Samia amemteua Profesa Eleuther Mwageni kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo CBE na Dk. Neema Mwita kuwa Mjumbe wa Baraza la Ushindani.

Taarifa hiyo imebainisha kuwa Profesa Mwageni ni Mhadhiri wa Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Ardhi (ARU) anachukua nafasi ya Profesa Ester Ishengoma aliyememaliza muda wake.

Katika taarifa hiyo imeeleza kuwa Rais Samia amemteua Dk.Neema Mwita kuwa Mjumbe wa Baraza la Ushindani anyechukua nafasi ya Dk.Theodora Mwenegoha aliyeteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania.

Aidha uteuzi huo umeanza leo Juni 8,2021.