
Mbunge wa Jimbo la Kavuu na Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe.Geophrey Pinda, amewataka wananchi wa jimbo hilo kutorudi nyuma katika kufanya kazi na kuwaeleza kuwa jimbo la Kavuu lipo juu hususan katika uzalishaji mazao kama vile mahindi na mpunga huku akiwaeleza wana jimnbo hilo kuisikia kauli ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan ya kazi iendelee.
Mhe.Pinda amesema Kauli ya kazi Iendelee ya Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan, inaakisi utekelezaji wa miradi mbalimbali kama vile ujenzi wa miundombinu ya barabara, daraja pamoja na uboreshaji huduma za afya kama vile ujenzi wa vituo vya afya, zahanati sambamba na upatikanaji wa huduma ya maji.
Mhe.Pinda ameeleza hayo wakati Mbunge wa Jimbo hilo alipokwenda kuwafariji wananchi waliopatwa na ugonjwa wa Kipindupindu katika eneo la Mwamapuli Halmashauri ya Mpimbwe mkoani Katavi.
Mhe.Pinda amewataka wananchi wa eneo hilo kuanza juhudi za kutokomeza ugonjwa huo kwa kuwa wasafi, pamoja na kuhakikisha kila nyumba inakuwa na choo.
Hata hivyo wananchi wa jimbo la Kavuu katika eneo la Mwamapuli katika halmashauri ya Mpimbwe mkoa wa Katavi wamekosa maswali ya kumuuliza Mbunge wa Jimbo hilo ambaye ni Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendekeo ya Makazi Mhe. Geophrey Pinda kutokana na kukamilisha asilimia kubwa ya ahadi alizozitoa wakati wa kampeni ya uchaguzi mwaka 2020.
Akiwa katika eneo hilo, Mhe.Pinda amewataka wananchi hao kufanya kazi kwa bidii na kuweka wazi kuwa inapoelezwa kuwa eneo la Mwamapuli lina changamoto aniatafuta kwa kuwa kazi kubwa ameifanya kulihudumia jimbo la Kavuu.
Mbunge wa Jimbo la Kavuu na Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Geofrey Pinda, alikuwa jimboni kwake kwa ziara ya siku moja ambapo alifanya shughuli mbalimbali kama vile ukaguzi wa barabara ya kilomita 70 Kibaoni – Sitalike, kukabidhi magari ya wagonjwa pamoja na kuwafariji wananchi waliopatwa na ugonjwa wa kipiundupindu kwenye eneo la Mwamapuli.