
Waziri wa Afya Mhe.Ummy Mwalimu amepongeza hatua iliyochukuliwa na Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala kwa kumsimamisha kazi Mtumishi wa afya, katika Kituo cha Afya Kivule baada ya kuonekana kwenye video, iliyosambaa kwenye mitandao ya kijamii ikimuonyesha mtumishi huyo, akisafisha vifaa tiba kwa njia isiyofaa.
.
Waziri Ummy ameyasema hayo, akiwa katika ziara ya kukagua ubora wa huduma za afya katika vituo vya kutolea huduma za afya, Bariadi, Mkoani Simiyu, huku akisisitiza kuwa alichofanya mtumishi huyo hakikubaliki hata kidogo.
.
Aidha Mhe.Ummy amewataka watumishi wa Afya kuzingatia weledi katika Majukumu yao ya kazi, huku akiwaagiza Wakuu wa Mikoa na Wilaya kuwachukulia hatua za kisheria watumishi wanaokiuka maadili na miiko ya majukumu yao.
