Back to top

MIGOGORO YA ARDHI: SILAA AAGIZA DIWANI AKAMATWE

21 January 2024
Share

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Jerry Silaa, amemuagiza Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Bw.Saad Mtambule, kuhakikisha anamkamata mtu anayejulika kwa jina la 'Diwani' ambaye anadaiwa kusababisha migogoro ya ardhi katika eneo la Mtaa wa Mbopo, lililopo Kata ya Bunju, mkoani Dar es Salaam.
.
Mhe.Silaa ametoa maagizo hayo, alipofanya ziara katika eneo la Mbopo, lililokuwa na mgogoro wa ardhi wa muda mrefu kati ya wakazi wa eneo hilo, ambao wanadaiwa kuwa ni wavamizi na Shirika la Uchumi la Jiji la Dar es Salaam (DDC), ambapo amefanikiwa kumaliza mgogoro huo, uliodumu kwa muda mrefu.
.
Aidha, Waziri huyo amewataka wakazi wa maeneo hayo kuacha kutumia watu ambao sio viongozi wa kisheria ambao wanawadanganya wananchi na kusababisha uvamizi.