
Miili 12 kati ya 13 iliyokuwa majini, baada ya mitumbwi miwili kuzama, katika Ziwa Victoria, katika Kijiji cha Mchigondo kilichopo wilayani Bunda, mkoani Mara, siku ya Jumapili ya Juni 30, 2023, ikiwa na watu 28, imeopolewa majira ya Saa 3 hadi saa 6 usiku na alfajiri ya leo, Agosti 02, 2023.
.
Akizungumza na ITV, Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Mkoa wa Mara, Augustine Magere amesema wanaendelea na juhudi za kutafuta mwili mmoja ambao bado haujapatikana.
