Miili ya watoto 3 wa familia moja waliopotea imekutwa ndani ya gari. 

Miili ya watoto watatu wa familia ya Bw.Mohamed Nongo,wawili wa kike wenye umri wa miaka 7 na mwingine miaka nane  huku mtoto wa  kiume akiwa na  umri wa mwaka mmoja imekutwa ndani ya gari aina ya Mark X ,baada ya watoto hao kupotea siku tatu zilizopita katika mtaa wa Njaro,wilaya ya Temeke jijini Dar Es salaam.

Kamanda wa polisi kanda maalum ya Dar es salaam Lazaro mambosasa amemtaji baba wa watoto hao kuwa ni Mohamed Nongo,na kwamba kwa maelezo ya awali inasemakana watoto hao walikuwa wakicheza jirani na lilipo gari hilo na inasadikiwa waliingia kwenye gari na kujifungia na hivyo kushindwa kutoka.