Back to top

Mikoa ya Njombe, Kigoma, Ruvuma na Rukwa inakabiliwa na udumavu.

17 October 2020
Share

Wizara ya Kilimo imesema kuwa mikoa mingi inayoongoza kwa uzalishaji wa chakula ikiwemo mkoa wa Njombe, Kigoma, Ruvuma na Rukwa inakabiliwa na adha ya udumavu hali inayoashiria kuwa wakazi wanahitaji kuhamasishwa kuzingatia lishe.

Akizungumza wakati wa kilele cha maadhimisho ya Siku ya Chakula Duniani ambayo kitaifa yalifanyika mkoani Njombe, Waziri wa Kilimo Mheshimiwa Japhet Hasunga amewataka wakazi katika mikoa hiyo kubadili desturi ya ulaji vyakula.

Hata hivyo, Katibu Mkuu wa wizara hiyo Bwana Gerald Kusaya amesema hali ya udumavu kitaifa inazidi kupungua huku magonjwa yasiyoambukiza yakiongezeka.

Wakazi wa mkoa wa Njombe waliozungumza na ITV wamesema udumavu mkoani humo unasababishwa wazazi na walezi ambao wanatumia muda mrefu kwa shughuli za kilimo na biashara, siyo uhaba wa chakula.