Back to top

Mipaka ya Uganda kufunguliwa kwa ajili ya watalii.

20 September 2020
Share

Rais Yoweri Museveni ameruhusu kufunguliwa kwa mipaka na uwanja wa ndege wa Entebbe,japo kwa watalii wenye vyeti vinavyoonyesha hawana maambukizi ya Corona chini ya saa 72.

Museveni pia ametangaza kwamba shule zitafunguliwa tarehe 15 Oktoba kwa wanafunzi Milioni 1.2 wanaotarajia kufanya mitihani ya mwisho.

Mpango wa kuwapa wanafunzi redio kulingana na Museveni upo katika maandalizi ya mwisho.

Maeneo ya ibada yatafunguliwa, watu wasiozidi 70 na waliovalia barakoa wakiruhisiwa kuhudhuria.

Michezo na michuano imeruhusiwa kuendelea mradi tu wachezaji wapimwe virusi vya corona chini ya saa 72, wakihitajika kuwekwa karantini kwa siku 14 baada ya mchezo.


Rais Museveni anasema kwamba haipo haja ya kurejesha marufuku aliyokuwa ameweka kudhibiti kuenea kwa homa ya COVID 19, akitangaza kwamba kila raia atabeba mzigo wake.