
Serikali mkoani Mtwara imesema miradi ya kimkakati iliyowekezwa na serikali yenye, thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 200 imefungua maendeleo katika mikoa ya Kanda ya Kusini lakini pia nchi jirani ya Msumbiji na Comoro.
Kauli hiyo ya Mkuu wa mkoa wa Mtwara, Kanali Ahmed Abbasi, baada ya kufanya ziara ya kutembelea miradi ya kimkakati iliyowekezwa na serikali kuu mkoani humo.
Amesema serikali ya awamu ya sita haina budi kupongezwa kwani imewekeza miradi yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 200 hivyo miradi hiyo haina budi kulindwa kwa gharama kubwa.
Amesema miradi hiyo ni chachu ya maendeleo katika mikoa ya Kusini na nchini jirani ya Msumbiji na Comoro katika kuhuisha maendeleo nchini.
Hata hivyo amesema baadhi ya changamoto zilizojitokeza katika miradi ikiwemo hospitali ya Kanda serikali itazifanyia kazi, ili miradi hiyo iweze kunufaisha wananchi na taifa kwa ujumla.