
Shirika la Umeme nchini (TANESCO) , limetoa taarifa kuwa kumetokea hitilafu kwenye mitambo yake ya Kinyerezi II iliyopo jijini Dar es Salaam, hali iliyopelekea megawati 131 kutokuwa kwenye mfumo wa usafirishaji umeme, na kusababisha baadhi ya mikoa nchini kukosa umeme, kuanzia majira ya asubuhi hadi mchana wa siku ya leo agosti 11, 2022.
.
Hata hivyo, Shirika hilo limebainisha kuwa, jitihada za kurekebisha hitilafu hiyo zinaendelea.

