
Rais wa Zanzibar Dkt.Hussein Mwinyi amewashukuru walimu wa shule zote kwa kazi wanayofanya kuhakikisha wanatoa elimu bora iliyozalisha matokeo mazuri.
Rais Mwinyi ametoa shukurani na pongezi hizo wakati wa hafla fupi ya chakula cha pamoja na wanafunzi wa kidato cha sita na Kidato na Nne waliofanya vizuri katika mtihani yao ya taifa ya mwaka 2023, katika viwanja vya Ikulu Pagali Pemba.
Rais Mwinyi amesema dhamira ya serikali ni kuimarisha miundombinu ya elimu na kuendelea kuongeza kiwango cha ufaulu kwa wanafunzi kupitia mageuzi yanayoendelea ambayo yamechangia kwa kiasi kikubwa ongezeko la ufaulu kwa wanafunzi wa kidato cha nne na kidato cha sita.
Rais Mwinyi ameahidi kuwapa Kompyuta mpakato (Laptop) wanafunzi wote waliopata daraja la kwanza ili kuwasaidia kufanya vizuri katika masomo katika ngazi nyingine.
