
Katibu Mkuu wa Chama cha Mabaharia Tanzania, Bw.Josiah Mwakibuja, ameiomba serikali kuhakikisha mkataba wa bandari hauathiri maslahi ya mabaharia wa ndani, na utoe fursa ya kufanya kazi kwa mabaharia hao ili wanufaike kama mabaharia wa nchi zingine.
.
Bw.Mwakibuja ameyasema hayo kwenye Kilele cha Wiki ya Mabaharia, ambayo kitaifa kilifanyika mkoani Mwanza.
