Back to top

MKATABA WA PUMA NA SOKA LA ISRAEL KUKOMA 2024

13 December 2023
Share

Kampuni ya vifaa vya michezo ya 'Puma' imetangaza kuacha kuifadhili timu ya Taifa ya Israel ifikapo mwaka 2024.
.
Kupitia taarifa iliyotumwa kwa barua pepe kwa shirika la habari la Reuters, Msemaji wa kampuni Puma amebainisha kuwa mikataba ya  kampuni hiyo na baadhi ya mashirikisho ikiwemo Serbia na Israel, itakoma ifikapo 2024 na kwamba mikataba hiyo haitaongezwa.
.
Ikumbukwe kwa muda mrefu Puma imekuwa ikishinikizwa kusitisha ushirika wake na Shirikisho la Soka la Israel (IFA), ambapo mashinikizo hayo yameongezeka zaidi tangu kuanza kwa mashambulizi ya Israel, huko Gaza, ambayo yamedaiwa kusababisha vifo vya zaidi ya Wapalestina 18,000.