
Afisa mmoja wa Polisi amefariki dunia huku wengine wawili wakijeruhiwa, baada ya kilipuzi kilichokuwa kimefichwa kwenye mkokoteni unaovutwa na Punda, kulipuka huko katika Kaunti ya Mandera nchini Kenya.
Polisi nchini humo wamesema mlipuko ulitokea siku ya Alhamisi majira ya 03:50 Asubuhi, baada ya tela hilo kusimama kwenye kizuizi cha Polisi kwa ajili ya ukaguzi.
.
Hata hivyo, Mamlaka za usalama nchini humo zimesema zinaendelea na uchunguzi juu ya tukio hilo, ili kujua nani alikuwa nyuma ya shambulizi hilo, huku baadhi ya taarifa zikidai kuwa mkokoteni huo uliokuwa ukivutwa na punda ulikuwa ukiongozwa na mtu anayedhaniwa kuwa ni mwanamgambo wa Al-Shabab na kwamba aliruka na kutoroka muda mfupi kabla ya mlipuko huo kutokea.

