Back to top

Mkufunzi mbaroni kwa kujihusisha na rushwa ya ngono na mwanafunzi.

08 April 2021
Share

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoani Kagera inamshikilia Bw.Cleophace Kyaragaine (59) mkufunzi wa Chuo cha kilimo Maruku kwa tuhuma ya kujihusisha na rushwa ya ngono kutoka kwa mmoja wa wanafunzi katika chuo hicho ambaye jina lake limehifadhiwa kwa lengo la kusaidiwa aweze kufaulu mitihani yake anayoifanya. 
.
Akizungumza na waandishi wa habari akiwa ofisini kwake, mkuu wa TAKUKURU katika mkoa huo Bw.John Joseph amesema mkufunzi huyo kosa alilotenda ni kinyume na vifungu vya 15 na 25 vya sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa namba 11 ya mwaka 2007. 
.
Aidha Mkuu huyo ameendelea kuwahimiza wananchi wajiepushe na vitendo vya rushwa kwa kuwa vinadhoofisha maendeleo ndani ya jamii hivyo akasema taasisi hiyo itaendelea mapambano ya kupinga rushwa ya ngono kwa nguvu zote.