Back to top

MKUTANO WA SADC NGAZI YA WATAALAMU ANGOLA.

09 August 2023
Share

Tanzania inashiriki Mkutano wa 43 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) uliofunguliwa leo tarehe 08 Agosti 2023 jijini Luanda, Angola kwa ngazi ya Maafisa Waandamizi ambapo ujumbe kutoka Tanzania unaongozwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Bi. Amina Shaban.

Wakati wa ufunguzi wa Mkutano huo Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) imekikabidhi uenyekiti wa ngazi hiyo, kwa Angola ambayo itashikilia wadhifa huo kwa kipindi cha mwaka mmoja hadi Agosti 2024.

Mkutano huo utakaofanyika takribani kwa siku 10 umegawanyika katika makundi mbalimbali ikiwa ni pamoja na Mkutano wa Kamati ya Fedha tarehe 10 Agosti 2023; Mkutano wa Baraza la Mawaziri tarehe 13 na 14 Agosti 2023; Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Ushirikiano wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama tarehe 16 Agosti 2023 na Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa SADC tarehe 17 Agosti 2023.