Back to top

Mkutano wa wadau wa korosho waahirishwa gafla Dar es Salaam.

18 September 2018
Share

Baadhi ya wabunge Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wakuu wa wilaya na wakurugenzi wa halmashauri kutoka katika  mikoa ambayo inalima korosho wamejikuta njia panda ya ama kubaki Dar es salaam au kurudi katika maeneo yao ya kazi baada ya mkutano uliokuwa umepangawa kufanyika kujadili zao la korosho kuahirishwa ghafla bila ya kupewa sababu au siku mbadala  ambayo mkutano huo utafanyika.

Aidha wabunge wengine wamesema hata kama kikao kingeahirishwa basi taratibu za kuahirisha kikao hicho zingefuatwa hata kwa kutumia ujumbe mfupi wa simu ya mkononi na siyo kusubiri watu wafike ndio mkutano uahirishwe.

Akitoa ufafanuzi wa tukio hilo Naibu Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na serikali za mitaa TAMISEMI Mh Joseph Kakunda amesema kikao hicho kimeahirishwa kwasababu kilitokea kikao kingine kikubwa zaidi.