Back to top

Mmiliki wa Mabasi akutwa gesti akiwa amekufa.

05 January 2020
Share

Mmiliki wa Mabasi ya Sahara yanayofanya Safari zake kutoka Usangi, Dar na Arusha, Bwana Abdallah Msangi mkazi wa Ndorwe Usangi amekutwa amefariki katika nyumba ya kulala wageni Moshi mkoani Kilimanjaro.

Kufuatia taarifa zilizotolewa na Jeshi la Polisi zinasema marehemu alikuwa na rafiki yake wa kike (jina lake halijafahamika) ambapo baada ya tukio hilo mwanamke huyo alikimbia.

Jeshi la polisi linaendelea na uchunguzi wa tukio hilo.