Back to top

Mmiliki wa mashamba makubwa Simanjiro akamatwa  na TAKUKURU.

16 October 2020
Share

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa mkoani Manyara (TAKUKURU)  inamshikilia mmiliki  wa mashamba makubwa kwa kutowalipa wafanyakazi wake  mishahara kwa miezi 11 ambao wamekua wakifanya kazi tangu novemba 2019 hadi Oktoba mwaka huu.
 
 
Kamanda wa TAKUKURU mkoa wa Manyara akizungumza na wanahabari amesema kuwa wamemkata mmliki huyo anayefahamika kwa jina la Thomas Meliyo baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa wafanyakazi wake.