
Jeshi la Polisi, Mkoa wa Geita limeanza uchunguzi wa tukio la gari la matangazo la Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kuchomwa moto na watu wasiojulikana saa nane za usiku wa kuamkia leo Agosti 02, 2023, wakati likiwa limeegeshwa katika ya hoteli ya Twiga, iliyopo wilayani Chato, mkoani Geita.
.
Akitoa taarifa hiyo Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani humo, ACP Adamu Maro, amesema tayari timu ya upelelezi imefika kwenye eneo la tukio na tayari wanamshikilia mtu mmoja ambaye ni mlinzi wa hoteli hiyo kwa mahojiano, huku akiwaonya watu wanaovuruga mikutano iliyoruhusiwa na serikali kuacha kwani Jeshi hilo halitamvumilia mtu yeyote anayeendesha uhalifu kupitia mikutano hiyo.