Back to top

Mmoja ajinyonga kwa mkanda,mwingine jaribio la kutoa mimba Kagera.

12 February 2020
Share

Watu wawili mkoani Kagera wafariki kwa nyakati tofauti akiwemo mwanafunzi wa darasa la sita katika shule ya msingi ya Kiilima  mkoani Kagera Alinda Revelian (14) aliyefariki wakati akijaribio kutoa mimba na Buberwa Mbelwa (13) mwanafunzi wa darasa la tano katika shule ya msingi ya Kahororo aliyejinyonga kwa mkanda wa suruali.

Kamanda wa Jeshi la polisi Kagera kamishina Msaidizi Revocatus Malimi amesema jeshi hilo linamshikilia Desder Solomoni Kahwa aliyewahi kuwa muuguzi kabla ya kutumbuliwa ambaye alikuwa akimpa msaada wa namna ya kutoa mimba hiyo na kwa sasa wanamtafuta  aliyempa mimba mwanafunzi huyo.

 Lakini pia Kamanda huyo ambaye ameendelea kuwahimiza wananchi katika mkoa huo wajiepushe na vitendo vya kuchukua uamzi wa kujiua baada ya kutingwa na msongo wa mawazo .