Back to top

Mnaoishi kwenye miiniko toeni taarifa mnapohisi dalili za Usubi.

12 September 2019
Share

Wataalam wa utafiti wa magonjwa ya binadamu nchini wamewataka wananchi hasa waishio maeneo yenye miinuko katika wilaya za Muheza,Ulanga na Tukuyu kuhakikisha wanatoa taarifa kwa wataalam wa afya pindi wanapohisi kuwashwa ngozi na kubadilika kuwa na mabaka.

Akizungumza jijini Tanga baada ya timu ya wataalam kutembelea maeneo hayo,Mtafiti wa taasisi ya uchunguzi wa magonjwa ya binadamu (NIMR) kituo cha Tanga Dk,Bruno Mmbando amesema utafiti uliofanywa umebaini kuwa ugonjwa wa usubi unaosababishwa na minyoo midogo kwenye mishipa ya damu bado ni changamoto katika maeneo hayo.

Awali akizungumza na waandishi wa habari kuhusu matokeo ya sayansi za utafiti msimamizi wa shughuli za uchapishaji na uandaaji makala za matokeo ya utafiti katika Tume ya taifa ya Sayansi na teknolojia Dk.Bakari Msangi amesema wameanza mchakato wa kuelimisha waandishi ili matokeo ya utafiti yaweze kuwafikia walengwa.

Ugonjwa wa USUBI husambazwa kwa kuumwa na nzi weusi(blackflies) aina ya  Simulium (Simulium species,ambaye hubeba vimelea vichanga kutoka kwa binadamu mmoja kwenda kwa mwingine.


DALILI


Ndani ya mwili wa binadamu vimelea hukua na kuzaliana kwa mingi (1000 kwa siku) ambavyo husambaa ndani ya mwili na baada ya kukua na kufa husababisha dalili zifuatazo;
Upofu (blindness)
Vipele vya ngozi (skin rashes)
vidonda (lesions)
miwasho (itching) na
kuchuchuka kwa ngozi (skin depigmentation)

KINGA NA TIBA


Katika mataifa mengi USUBI hukingwa kwa kuua weusi kwa dawa ya kupulizia (insecticides) , pia kwa kuua vimelea kwa dawa iitwayo Ivermectin, ambayo hutolewa dozi moja kwa njia ya mdomo na hurudiwa kila baada ya miezi sita mpaka kumi na mbili mpaka dalili zitakapo isha.