Back to top

Mo Dewji ataja sababu za kujiuzulu Simba.

29 September 2021
Share

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Simba, Mohammed Dewji amejiuzulu nafasi hiyo baada ya kuitumikia kwa muda wa miaka minne.

Mo Dewji nafasi yake imechukuliwa na Abdallah Salim (Try again).

Kupitia Ukurasa wa Twitter Mo dewji ametaja sababu za kujiuzulu nafasi hiyo ikiwemo majukumu yanayomfanya asafiri mara kwa mara na kusema nafasi hiyo inahitaji mtu ambaye yupo wakati wote.

Mo Dewji amewataka wanasimba wasiwe na hofu kwani yeye bado ni mwanasimba na daima ataipenda Simba na bado ni mwekezaji wa klabu hiyo.

"Naomba sana wanasimba msifikirie kwamba mimi nimeondoka kwenye Simba, bali bado ni mwekezaji kwenye Simba, naipenda Simba na nitaendelea kupenda Simba mpaka siku yangu ya mwisho".Mo Dewji.