Back to top

MOI yafanya upasuaji mkubwa maalum wa kubadilisha Nyonga.

28 March 2018
Share

Taasisi ya mifupa MOI yafanya upasuji mkubwa maalum wa  kubadilisha kiungo cha Nyonga kwa mgonjwa madaktari bingwa wa taasisi ya mifupa Muhimbili kwa kushirikiana na daktari bingwa wa mifupa kutoka hospitali ya Prashanth Chenai ya nchini India wamefanikiwa kufanya upasuaji mkubwa na mgumu wa kibingwa wa kubadilisha kiungo cha Nyonga cha mgonjwa huduma ambayo haijawahi kufanyika toka kituo hicho kuanzishwa.

Upasuaji huo umefanywa na jopo la madaktari bingwa wanne ambao wameongozwa na Dkt. Mani Ramesh kutoka India na Dkt.Samweli Kitugi Nungu wa MOI ambapo upasuaji huo umefanyika kwa ufanisi na  kwa masaa matatu.

Akizungumza baada ya upasuaji huo mkurugenzi mtendaji wa MOI Dkt.Respicious Boniface amesema ujio wa daktari kutoka India ni sehemu ya mkakati wa taasisi ya MOI kuwajengea uwezo wataalamu wake kwa kupata mbinu mpya kutoka kwa wataalamu kutoka nchi mbalimbali.

Kwa upande wake Dkt.Ramesh kutoka India amesema amefarijika kwa namna MOI wanavyotoa huduma zao na kuongeza kuwa jambo la msingi ni taasisi hiyo kuendelea kujijenge uwezo ili kuweza kuwafikia watu wengi zaidi.

Nimefarijika sana kwa siku tano nilizokaa hapa Tanzania, tumeshirikiana na kubadilishana uzoefu kwenye matibabu haya ya kibingwa ya nyonga, binafsi naamini huu ni muendelezo mzuri wa ushirikiano kati ya moi na hospitali yetu ya Prashant naamini nitarajea tena hapa''

MOI imeweza kufanikisha yote haya kutokana na serikali ya awamu ya tano kutoa fedha za kununulia vifaa tiba na kuboresha miundo mbinu kwa ajili ya kutolea huduma hizo.