Back to top

Mongella aamuru M/Halmashauri Sengerema na Afisa ardhi kuwekwa ndani

05 January 2021
Share

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella ameamuru kuwekwa ndani kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Sengerema Bw.Boniface Magesa na Afisa Ardhi wake kwa kutoa taarifa za uongo kwa Mkuu wa wilaya ya Sengerema na mkuu wa mkoa wa Mwanza.

Mongella ametoa amri hiyo baada ya Waziri wa TAMISEMI, Selemani Jafo kusikiliza kilio cha mkazi wa Sengerema, Christopher Derefa kudai kudhulumiwa fedha za malipo ya fidia.

"Ningekuwa na mamlaka leo hii ningewaweka ndani mkurugenzi na bwana ardhi hata kwa saa tatu tu"-Jafo