
Afisa ustawi wa jamii, Wilaya ya Temeke, Theresia Nkwanga, amwataka walimu wa watoto wadogo kutobaki au kulala na watoto baada ya muda wa shule kuisha (saa 10-12jioni) badala yake wanatakiwa kuripoti katika ofisi za serikali ya mitaa na afisa ustawi wa jamii ikiwa wazazi wa watoto hao wanachelewa kuwachukua.
Akihutubia wakati wa maadhimisho ya siku ya Mtoto wa Afrika kwa walimu na wanafunzi wanatumia mtaala wa Montessori Afisa Ustawi wa Jamii huyo amewataka walimu kutokubali kulala na watoto ambao wazazi wao hawajawachukua baada ya muda wa masomo badala yake kutoa taarifa kwa maofisa Ustawi wa Jamii.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Taasisi ya Montessori Sarah Kiteleja amewaasa walezi kuzingatia malezi ya Kiafrika na kuongeza kwamba mbinu ya kufundishia ya Montessori ambayo inazingatia vitendo zaidi na michezo, inafanana na mazingira ya mtoto wa Kitanzania.



