Back to top

Moto ulioteketeza soko la Samunge jijini Arusha waua mfanyabiashara 1

29 March 2020
Share

Soko la wafanyabishara wadogo jijini Arusha linalijulikana kama Soko la Samunge limeteketea kwa moto usiku wa kuamkia leo na kusababisha  hasara  kubwa  ya Mamilioni ya fedha.

Mkuu wa wilaya ya Arusha, Bwana Gabriel Dakharo amesema moto huo ulianza majira ya saa tano usiku bado chanzo chake hakijajulikana na asilimia kubwa ya mali za wafanyabiashara zimeteketea.

Hata hivyo Bwana Dakharo amesema vyombo vinavyohusika vimeanza uchunguzi na pia kufanya tathmini ya hasara iliyopatikana na pia kuwatambua wenye mali husika na kwamba taarifa kamili tatolewa.

Kutokana na tukio hilo mtu mmoja aliyetajwa jina la James Peter Temba 57 amefariki dunia baada ya kupata mshituko uliotokna na mali  zake kuteketea kwa moto.

Kaimu Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Arusha, Bwana Koka Moita amethitisha kutokea kwa kifo cha mfanyabishara huyo na amesema  wanaendelea kuchunguza na pia kufuatilia zaidi madhara yaliyotokana na moto huo.