Back to top

Moto unaoendelea kuwaka Msitu wa Amazoni wateketeza hekta 1700

09 September 2019
Share

Moto unaoendelea kuwaka katika msitu wa Amazon nchini Brazil umevuka mpaka na kuteketeza hekta elfu moja na mia saba za misitu nchini Bolivia.

Ofisa wa Idara ya Misitu ya eneo la Santa Cruz nchini Bolivia Cinthia Asin amesema, moto huo umeteketeza zaidi maeneo ya hifadhi ya taifa na ameitaka serikali ya Bolivia kutangaza motio huo kuwa ni janga la taifa.

Amesema moto huo umeangamiza kabisa sehemu kubwa ya misitu ambayo ina vyanzo muhimu vya maji.

Mwishoni mwa mwezi Agosti mwaka huu serikali ya Bolivia ilitumia ndege aina ya Boeing 747 na ndege nyingine kadhaa ndogo kwa ajili ya kuzima moto huo.