Back to top

Moto wateketeza Bweni la shule ya Sekondari Kwa Uso mkoani Kagera.

30 July 2020
Share

Moto mkubwa ambao chanzo chake hakijajulikana umezuka katika Shule ya Sekondari ya Kwa Uso inayomilikiwa na Kanisa Katoliki Jimbo la Bukoba mkoani Kagera na kuteketeza kabisa vyumba vinne vya kulala vinavyotumiwa baadhi ya wanafunzi wa kike wanaosoma katika shule hiyo na walezi wakiwemo watawa.

Moto huo ambao umeteketeza mali zote za wanafunzi 67 zilizokuwa ndani ya vyumba hivyo umezuka majira ya saa tatu usiku wakati wanafunzi walipokuwa wakijisomea.

Kwa upande wake Afisa wa Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji Mkaguzi Thomas Majuto akizungumza amesema moto huo haukudhibitiwa mapema kutokana na  gari lililokuwa linaelekea kwenye eneo la tukio kuharibika wakati likiwa njiani.

Mkuu wa wilaya ya Bukoba Deodatus Kinawilo ambaye  ni miongoni mwa viongozi wa serikali waliotembelea eneo la tukio na kuongea na wanafunzi akizungumza ametoa pole  na ameviagiza vyombo vya ulinzi na usalama vichukue hatua za haraka za kubaini chanzo cha moto huo.