Back to top

Moto wateketeza kanisa kongwe la Notre-Dame mjini Paris Ufaransa.

16 April 2019
Share

Moto mkubwa umezuka katika kanisa kongwe la Notre-Dame mjini Paris Ufaransa ambalo ni moja ya makanisa maarufu na linalotembelewa na idadi kubwa ya watalii kutoka sehemu mbali mbali duniani 

Vikosi vya zimamoto vinaendelea kuzima moto huo katika kanisa hilo lililodumu kwa takriban miaka 850.

Sehemu kubwa ya paa la majengo ya kanisa hilo limeteketezwa na mto huo huku moto katika minara miwili ya kengele umefanikiwa kuzimwa.
 
Chanzo cha moto huo hakijajulikana, lakini maafisa maafisa wanauhusisha mkasa huo na shughuli ya ukarabati inayoendelea.

Wazima moto wanafanya kila juhudi kuokoa vito vya thamani vilivyoko ndani kanisa hilo na pia kuzuia mnara wa upande wa kasskazini kutoporomoka.
Maelfu ya watu wamekusanyika katika barabara zilizo karibu na kanisa hilo kushuhudia mkasa huo wakiwa kimya.

Baadhi yao walionekana wakidondokwa na machozi, huku wengine wakiimba nyimbo za sifa na kumuomba Mungu.