Back to top

MOTO WAUA WATU 20 HUKO NCHINI UGIRIKI

28 August 2023
Share

Wafanyakazi wa Kikosi cha Zimamoto na uokoaji nchini Ugiriki, wanaendelea kupambana kuzima moto mkubwa katika mikoa ya Evros na Alexandroupolis Kaskazini Mashariki mwa nchi hiyo, ambao hadi sasa umesababisha zaidi ya vifo ishirini.

Zaidi ya wafanyakazi 600 wakiwemo kutoka nchi kadhaa za Ulaya, wakisaidiwa na ndege kadhaa zinazomwaga maji wanapambana na moto uliozuka katika maeneo matatu ya msituni unaoendelea nchini Ugiriki.

Moto mwingine mkubwa unaendelea kuwaka kwa siku kadhaa kwenye miteremko ya mlima Parnitha, kwenye ukingo wa Kaskazini-Magharibi mwa mji mkuu wa Ugiriki, Athens, wakati moto wa tatu ulioanza Jumamosi iliyopita kwenye kisiwa cha Cycladic cha Andros unaendelea kuwaka bila udhibiti.