Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Philip Isdor Mpango, amesema serikali imejipanga kikamilifu katika kusimamia maadili, uawajibikaji na utawala wa sheria katika kuinua uchumi wa viwanda kwa maendeleo ya watu kama ilivyoelekezwa katika mpango wa tatu wa maendeleo ya taifa wa miaka mitano.
Makamu wa Rais ameyasema hayo jijini Dodoma wakati wa ufunguzi wa mkutano wa nne wa mtandao wa maombi ya asubuhi ya kitaifa na kimataifa na kusema kuwa serikali itaendelea kushirikiana na viongozi wa dini katika kuhakikisha kuwa Taifa linakuwa na ustawi bora kwa watu wake.
Aidha Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Rais Dkt Philip Mpango, ameeleza kuwa maombi hayo ni kiunganisho baina ya wanadamu na Mungu wao na kama watoto wa Mungu katika Kupendana na kuwajibika katika kuwatumikia watu wake.