Back to top

MPIMBWE YAPENDEKEZWA KUWA WILAYA

20 February 2024
Share

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi na Mbunge wa Jimbo la Kavuu, katika Halmashauri ya Mpimbwe katika wilaya ya Mlele mkoa wa Katavi Mhe.Geophrey Pinda, ameshiriki Kikao cha Kamati ya Ushauri ya Maendeleo ya mkoa- RCC, ambapo Halmashauri ya Mpimbwe imependekezwa kuwa Wilaya kamili.

Kikao hicho mbali na mambo mengine kilijadili na kupitisha Bajeti ya mkoa wa Katavi na Halmashauri zake kwa mwaka 2024/2025 pamoja na maeneo ya utawala.

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Geophrey Pinda, yuko mkoani Katavi ambapo atashiriki Mkutano Mkuu wa Jimbo la Kavuu katika halmashauri ya Mpimbwe wilaya ya Mlele mkoa wa Katavi.

Katika mkutano huo utakaofanyika Februari 24, 2024 katika Shule ya Sekondari Nizengo Pinda-Kibaoni Taarifa ya Utekelezaji wa Ilani ya CCM kuanzia Nov 2020 hadi Februari 2023 itawasilishwa na Mhe. Pinda.

Mgeni rasmi katika mkutano huo utakaofanyika anatarajiwa kuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa.