Back to top

Mpina aagiza kuchukuliwa hatua kwa wanaosababisha vifo vya mifugo.

06 July 2020
Share

Waziri wa Mifugo na Uvuvi  Mhe Luhaga Mpina ameiagiza Bodi ya Baraza la Veterani nchini kuwachukulia hatua watendaji na wataalamu wa sekta ya mifugo wanaofanya hujuma kwa kukamata ng’ombe  bila kuwapatia huduma muhimu ikiwemo maji na malisho hali iliyosabisha mifugo mingi kufa huku mingine ikiuzwa kiholela katika baadhi ya maeneo na kusababisha hasara kwa wafugaji.

Mhe Mpina ametoa maagizo hayo jijini Dodoma wakati akizindua Bodiya Wakala wa Vyuo vya Mafunzo ,Bodi ya Hifadhi ya Bahari na  Maeneo Tengefu na Bodi ya Baraza la Veterani Tanzania .

Aidha Waziri Mpina amepiga marufuku vishoka wanaotoa huduma za afya kwa mifugo ambapo amesema hatua za kisheria zitachukuliwa kwa watakaobainika.